Soma Biblia Kila Siku 6Mfano
Wakareja mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani (m.21-22). Hapa mtume Paulo atuonyesha mfano mzuri jinsi ya kufanya kazi ya uinjilisti. Hakuridhikakwa kuona tu watu wameokoka! Kuokoka ni mwanzo tu wa safari kwenda Mbinguni. Wakigeuka au kuchoka njiani bila kufika mwisho wa safari, kuna faida gani? Paulo alitaka ushindi wa Mungu katika maisha ya watu udumu hadi mwisho! Wala shetani asipate kujiinua kwa kupata ushindi wa mwisho. Petro aliandika: Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye; lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi. Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka(1 Pet 5:1-4).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz