Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 6Mfano

Soma Biblia Kila Siku 6

SIKU 27 YA 30

Maono haya ni mwendelezo wa Dan 7:1-12. Danieli anatafsiriwa kuwa wanyama wanne watishao wanawakilisha watawala watakaotokea katika dunia kwa wakati wake. Lakini asifadhaike kwa sababu ya nguvu zao, maana ni za muda tu. Mtawala wa kudumu ni mwanadamu ajaye kupitia mawinguni. Ni mwenye mamlaka juu ya mataifa yote. Huyu ni Yesu Kristo (m.13-14, Mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa; Mt 24:30, Ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi). Atawashirikisha watakatifu ufalme wake. Watakatifu hawa ni waumini wote wa taifa la Israeli pamoja na Kanisa (ling. m.18 na Lk 12:32, Watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme).

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz