Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 6Mfano

Soma Biblia Kila Siku 6

SIKU 24 YA 30

Paulo anaeleza wazi juu ya utumishi wake huko Efeso alikokaa sana. Alikuwa amemtumikia Bwana kwa ukunjufu wa moyo. Alikuwa mnyenyekevu kwa wito wake. Aliuheshimu sana wito wake. Zingatia m.24: Siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu. Jambo kubwa kwa Paulo lilikuwa kwamba kazi ya Bwana ifanikiwe wala si mambo yake binafsi (20:33-35, Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.Ninyi wenyewe mnajua ya kuwa mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea). Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu(m.27). Yaani hakuwafundisha mambo machache tu ya neno la Mungu bali ujumbe mzima, ili wawe na imani safi (m.20). Tuufuate mfano wake! Kumbuka Yesu alivyosema: Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha(Lk 9:23-24).

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz