Soma Biblia Kila Siku 6Mfano
Paulo yupo kwenye safari yake ya tatu ya misioni. Alipokuwa anamalizia safari ya pili alipitia kanisa mama Yerusalemu (akapanda juu, Mdo 18:22). Na baada ya kukaa nyumbani Antiokia kwa muda kidogo; akaondoka, akanza safari ya tatu. Alifika Efeso kama alivyokuwa ameahidi (18:21,Paulo aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso. 19:1, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko). Efeso ulikuwa ni mji mkuu katika eneo lile la Asia. Mji mkuu kwa idadi ya watu na pia kwa mambo ya dini na siasa. Huko Paulo alifundisha Injili kwa bidii kwa miaka miwili na miezi mitatu bila kuzuiliwa. Na matunda yakawa makubwa. Rudia m.10-12 na 17-20 ukizingatia ujumbe wake: Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida;hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake, magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka. ... hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa. Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao. Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu. Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz