Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 6Mfano

Soma Biblia Kila Siku 6

SIKU 18 YA 30

Maana alikuwa ana nadhiri (m.18b). Paulo ni Myahudi na wakati fulani alifuata desturi za Kiyahudi zilizofundishwa na Musa (k.m. 21:26, Siku ya pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu, akitangaza habari ya kutimiza siku za utakaso, hata sadaka itolewe kwa ajili ya kila mmoja wao). Kama ukitaka kufahamu zaidi kuhusu tendo la kutoa nadhiri (ahadi), unaweza kusoma Hesabu 6:1-21. Mstari wa 5 wasema: Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimfikilie kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa Bwana, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake sikue ziwe ndefu. Kuhusu umuhimu wa kazi ya Apolo huko Korintho (eneo la Akaya, m.27), tafakari ilivyoandikwa katika 1 Wakorintho 3:4-9,Hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa.Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz