Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!Mfano

Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!

SIKU 2 YA 7

“Funguo za   Uhusiano Uliofanikiwa”

Kila   uhusiano, iwe ni rafiki, mwanafamilia, mwenza, au hata Mungu, una mambo   mawili ya msingi kuufanya ufanikiwe: upendo na mapenzi  yanawashirikisha watu hao, na kuuweka upendo   huo katika matendo. 

Ukweli ni   kwamba upendo wa kweli siku zote utaambatana na matendo; rafiki wa kweli   anapomuona mwenzake ana mahitaji ataitikia kwa kumsaidia.  Hivyo hivyo ni kweli katika mahusiano yetu   na Mungu. Kumpenda Mungu kwa dhati huendana na matendo; kugusa moyo wa Mungu   kwa kugusa maisha ya watu wanaotuzunguka. 

Kuwa na   mahusiano bora na wengine huanzia na uhusiano wetu na Mungu. Ukweli ni   kwamba, Mungu anataka uhusiano wetu na wengine uwe ni tawi la uhusiano wetu   na Yeye. 

Kama   waamini, uhusiano wetu na Mungu (kwenda juu) na uhusiano wetu na watu (sisi   kwa sisi) ndio mambo muhimu kwa Mungu – kumpenda Yeye na kuwapenda wengine.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!

Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2