Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mpe Mungu Nafasi ya KwanzaMfano

Mpe Mungu Nafasi ya Kwanza

SIKU 4 YA 5

“Kushinda   Mapambano ya Maisha kwa Msaada wa Mungu”

Kuna   mapambano ya maisha siku zote yanayokabili maisha yetu. Upande mmoja ni   mashinikizo asili ya zamani ya dhambi – zile tabia za zamani, tamaa na dhambi   ambazo zimekuwa vigumu kwetu kuzishinda. Muda unavyoendelea tunavyozidi kukomaa   katika mwendo wetu na Mungu, shinikizo la asili ya dhambi hupungua nguvu.   Upande mwingine ni kukua kwa utawala wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu.   Hizi ni nguvu mbili zinazopingana kama inavyobainishwa katika Wagalatia: 

“Basi   nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa   sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa   maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.” Wagalatia 5:16-17

Neno la   Mungu linatuhamasisha sisi “kuishi kwa Roho.” Kwa maneno mengine, ni lazima turuhusu umiliki wa Roho Mtakatifu ili   kushinda juu ya mashinikizo ya asili ya dhambi katika mkaisha yetu. 

Mara nyingi, hili ni rahisi kusema kuliko kulitenda.   Asili yetu ya dhambi hutusukuma kufanya uamuzi kutosheleza shauku zetu zenye ubinafsi. Hii huitwa   kujaribiwa, na Yakobo analielezea namna hii: 

“Mtu ajaribiwapo, asiseme Ninajaribiwa na Mungu; maana   Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini   kila mmoja wetu hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na   kudanganywa.” Yakobo 1:13-14

Ni mpaka pale uamuzi unapofanyika kwa upande wetu wa   kujiachia kuingia katika tamaa ndipo huko kujaribiwa hugeuka kuwa dhambi. 

“Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi,   na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.” Yakobo 1:15

La kushangaza, ikiwa ni sehemu ya upendo wa Mungu   usioelezeka na neema yake kwa Wakristo wote, Mungu hutusamehe na kutusafisha   kutoka katika dhambi zetu zote. Sisi tumesamehewa kabisa kwa  100% . 

“Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki   hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” I Yohana 1:9

Lakini   bado iko hatari ya kutojilinda na dhambi. Pamoja na kwamba Mungu anatusamehe   na kutuosha, hafuti ile njia ya uharibifu na mazingira ambayo matokeo ya   dhambi huacha nyuma.  Wakati ambapo   Mungu hutusaidia katika wakati mgumu, hata kama ni maamuzi yetu sisi wenyewe   ndio yaliyosababisha, njia bora ya maamuzi kwetu ni kujizuia kufanya maamuzi   yaletayo dhambi. 

I Wakorintho   inaelezea mambo mawili muhimu ya kushughulika kwa ufanisi juu ya tamaa na   dhambi: 

“ Jaribu   halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni   mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile   jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.” I Wakorintho   10:13

Kwanza   ujue kwamba hauko peke yako katika hayo mapambano. Ufahamu kuwa Wakristo   wenzako nao wanapitia hayo, aidha iwe ni siku 30 au miaka 30 ya kutembea kwao   na Mungu, bado wanapambana na dhambi na majaribu kama unayokabiliana nayo   wewe. 

Pili, ni   kwamba Mungu hataruhusu tujaribiwe hata kufika mahali ambapo hatuwezi kufanya   uamuzi wa kushinda dhambi. Wakati wote atatufanyia njia ya kushinda. Kazi   yetu, hata ikiwa ngumu kiasi gani, ni kupata njia ya kutoka katikati ya   majaribu yanayotukabili. 

Sehemu   inayofuatia inatoa mkakati wa Ki-Biblia wa kushughulikia dhambi na majaribu   kwa ufanisi. Kuutumia mpango huu ni njia moja zaidi ya kumpa Mungu nafasi ya   kwanza katika maisha yako!

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Mpe Mungu Nafasi ya Kwanza

Kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yetu si tukio la mara moja . . .ni mchakato wa maisha kwa kila Mkristo. Uwe ni Mkristo mpya au mfuasi wa Kristo “wa miaka mingi”, utagundua kuwa mpango huu ni rahisi ku - uelewa na ku - utumia, na ya kuwa ni mkakati wenye ufanisi wa hali ya juu kwa maisha ya ushindi ya Kikristo.

More

Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2