Mpe Mungu Nafasi ya KwanzaMfano
"Mungu Amekupa Wewe Nafasi ya Kwanza Moyoni Mwake”
Utafikiria nini kama mtu akikuambia kwamba Mungu anakuona wewe kama mtu ambaye hukuwahi kutenda dhambi? Ukweli ni kwamba, kwa sababu ya kazi ya ukombozi ya Yesu Kristo pale msalabani, hivyo ndivyo Mungu akuonavyo. Kama Wakristo, tumesamehewa, tumeoshwa, na tu huru!
Hii inamaanisha kuwa wewe ni mtakatifu: mtu aliyefanywa mwenye haki katika Kristo. Wewe ni mkamilifu, mtakatifu na asiye na waa katika macho ya Mungu. Anakuita wewe mwana Wake, mrithi wa utajiri wake, na rafiki Yake.
"Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu." I Petro 2:9
Kuelewa kwa usahihi jinsi Mungu anavyotuona inaanzia na jinsi sisi tunavyomuona Mungu. Mungu haangalii kwa kutoka mbali akitusubiri sisi kufanya makosa ili atuadhibu. Huu ndio ukweli.
Angalia mstari huu unasema nini:
"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake, - waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu." Yohana 1:12-13
Mungu humuona kila mmoja wetu kama mtoto Wake wa thamani. Yeye ni Baba mpendwa anayetupa kibali na kutujali kwa huruma zake zisizo na kikomo. Baadhi ya maandiko katika Wimbo Ulio Bora yanaonyesha huo upendo wa ajabu wa Mungu kwetu kwa kulinganisha na upendo wa mume na mke. Waebrania 11:6 inatuambia kwamba Mungu huwapa thawabu wale wamtafutao.
Mungu humuona kila mmoja wa watoto Wake katika njia tofauti kabisa ya jinsi sisi tunavyojiona. Kuelewa jinsi Mungu amuonavyo kila mmoja wetu huonekana katika kazi ambayo Kristo huanza katika maisha yetu mara tu tunapopokea wokovu.
"Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya." II Wakorintho 5:17
"Yeye asiyejua dhambi alimfanya dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye." II Wakorintho 5:21
Kufanywa kiumbe kipya ni kazi ya kiungu ya Mungu; kubadilishwa kabisa kwa hali yetu ya kiroho na utu wa ndani. Ametusamehe kabisa na kutusafisha kutoka dhambi zetu – za zamani, sasa na baadae. Sasa tuna mahusiano sahihi na Yeye.
"…Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi." Zaburi 103: 12
Tu watu wa Mungu tusio na waa lolote la dhambi;walio wenye haki Wake kupitia kazi aliyofanya Yesu msalabani. Hakika Mungu ametupa nafasi ya kwanza moyoni Mwake!
Kuhusu Mpango huu
Kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yetu si tukio la mara moja . . .ni mchakato wa maisha kwa kila Mkristo. Uwe ni Mkristo mpya au mfuasi wa Kristo “wa miaka mingi”, utagundua kuwa mpango huu ni rahisi ku - uelewa na ku - utumia, na ya kuwa ni mkakati wenye ufanisi wa hali ya juu kwa maisha ya ushindi ya Kikristo.
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2