Mpe Mungu Nafasi ya KwanzaMfano
“Mungu Anataka Nafasi ya Kwanza Moyoni Mwako”
Katika jamii ya leo, wengi huweka uthamani wao katika utajiri, wako juu kiasi gani katika kazi, jinsi gani wamefanikiwa kibiashara au wanamjua au kujulikana na nani?
Lakini ikiwa mtazamo wetu juu ya umuhimu unasimamia mambo haya, tutajisikia vizuri tu pale tutakapofanikiwa katika maeneo hayo. Utajiri wetu na mafanikio vitakapoporomoka, kujithamini kwetu nako pia kutashuka kwa kuwa msingi wetu si thabiti. Yesu anaelezea hili kama ifuatavyo:
“Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.” Luka 6:49
Utambulisho wetu unaendana na msingi tunaoweka juu yake. Kwa kuweka utambulisho wetu juu ya msingi wa mwamba imara Yesu Kristo, hali yetu ya utoshelevu katika maisha haitategemea hali inayobadilika ya vitu vya muda mfupi.
Kriso anapokuwa msingi wetu, uthabiti wetu ni kama huu:
“Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.” Luka 6:48
Fikiria kwa muda juu ya uchaguzi mwingi wa maamuzi unaokuwa nao katika maisha kujenga msingi wa maana. Hii inaweza kuhusisha mali, kazi, mwonekano, familia, nguvu au mtu unayemjua. Je kuna mengine unayoweza kuyafikiria? Juu ya vitu vyote tunavyoweza kuweka utambulisho wetu kwavyo, ni Yesu pekee ndiye anayetuhahakishia maisha ya ushindi ya Kikristo.
Lakini ukichunguza uchaguzi mwingine, hakuna ulio mbaya au uliojaa uovu. Uhalisia ni kwamba, mara nyingi, kuna maeneo mengi muhimu ya wajibu ambayo Mungu ametupa katika maisha yetu. Lakini katika kitabu cha Mathayo, Yesu anatusaidia kufahamu la kufanya.
“Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?” Mathayo 6:25-26
Tunapogundua ukweli huu katika maisha yetu binafsi, tunapata amani na utoshelevu, na kuwa huru kutoka katika hofu na mashaka. Hali hii inafikiwa tunapomweka Yesu kuwa nambari moja katika maeneo yote ya maisha yetu.
“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Mathayo 6:33
Sisi wote tuna ndoto, malengo na matamanio kwa kuwa ametuumba hivyo. Lakini kumweka Yesu kwanza hukufanya uchunguze vipaumbele na matamanio kwamba kwa nini utamani kufanya au kupata mambo unayotaka. Anapokuwa ni wa kwanza katika ndoto na matamanio yako, maisha yako yatajaa furaha na ukuu!
Mungu anapoleta jambo linalotatiza moyo wako, mwitikio wako muhimu unapaswa kuwa aliye tayari kufanya mabadiliko. Mabadiliko yanaweza kuwa kitu kigumu wakati mweingine, lakini siku zote Mungu anatuwazia jambo linalofaa, na anataka wewe ukue kiroho.
Kuhusu Mpango huu
Kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha yetu si tukio la mara moja . . .ni mchakato wa maisha kwa kila Mkristo. Uwe ni Mkristo mpya au mfuasi wa Kristo “wa miaka mingi”, utagundua kuwa mpango huu ni rahisi ku - uelewa na ku - utumia, na ya kuwa ni mkakati wenye ufanisi wa hali ya juu kwa maisha ya ushindi ya Kikristo.
More
Tungependa kuwashukuru Twenty20 Faith, Inc. kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.twenty20faith.org/yvdev2