Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kwa nini Pasaka?Mfano

Why Easter?

SIKU 5 YA 5

Ni nini ambacho ni lazima tufanye?  

Agano Jipya linadhihirisha kwamba ni lazima tufanye kitu ili tukubali zawadi ambayo Mungu anatupa. Hiki ni kitendo cha imani. Yohana anaandika kwamba ‘Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.' (Yohana 3:16).

Kuamini ni kitendo cha imani, ambacho kina msingi wa yale yote ambayo tunajua kuhusu Yesu. Kuamini huko si imani bila uthibitisho bali ni kuweka tumaini letu katika Mtu. Kwa njia nyingine, ni kama hatua ya imani ambayo maharusi wanachukua wanapokubali viapo vya ndoa katika harusi yao.

Njia ambayo watu wanachagua kuchukua hatua hii ni tofauti mno, lakini nataka kufafanua njia moja ambayo unaweza kuchukua hatua hii wakati huu. Muhtasari wa njia hii ni maneno matatu sahili:

‘Samahani’

Ni lazima umwombe Mungu msamaha kwa makosa yako yote na uache kitu chochote ambacho unajua ni makosa maishani mwako. Hii ndiyo maana ya neno ‘toba' katika Biblia.

‘Asante’

Tunaamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu msalabani. Unahitaji kumshukuru kwa kukufia na kwa kukupa kipawa cha bure cha msamaha, uhuru na Roho wake.

‘Tafadhali’

Mungu hajilazimishi maishani mwetu. Unahitaji kukubali kipawa chake na kumwalika aje na kuishi ndani yako kwa Roho wake.

Kama ungependa kuwa na uhusiano na Mungu na u tayari kusema hivi vitu vitatu, basi pana sala rahisi ambayo unaweza kusali na itakuwa mwanzo wa uhusiano huo:

Bwana Yesu Kristo,

Najuta vitu ambavyo nimetenda maishani mwangu ambavyo ni vibaya (chukua muda mfupi kumwomba msamaha kwa kosa lolote ambalo lipo dhamirini mwako). Tafadhali nisamehe. Naacha vitu vyote ambavyo ninajua ni vibaya.

Asante kwa kuwa ulikufa msalabani kwa ajili yangu ili nisamehewe na kuwekwa huru.

Asante kwa kuwa unanipa msamaha na kipawa cha Roho wako. Ninapokea kipawa hicho.

Tafadhali njoo moyoni mwangu kwa Roho wako Mtakatifu ukae nami milele.

Asante, Bwana Yesu. Amina.

Andiko

siku 4

Kuhusu Mpango huu

Why Easter?

Pasaka ina umuhimu gani? Mbona kuna shauku sana kuhusu mtu aliyezaliwa miaka 2,000 iliyopita? Mbona watu wengi wanachangamka kuhusu Yesu? Kwa nini tunamhitaji? Kwa nini alikuja? Kwa nini alikufa? Kwa nini mtu asumbuke kujua haya? Katika mpango huu wa siku tano, Nicky Gumbel anatoa majibu ya kuvutia kwa maswali hayo.

More

Tungependa kuwashukuru Alpha na Nicky Gumbel kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://alpha.org/