Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kwa nini Pasaka?Mfano

Why Easter?

SIKU 2 YA 5

Kwa nini alikuja, na kwa nini alikufa?

Yesu ni mwanadamu pekee aliyewahi kuchagua kuzaliwa, na ni Mmoja kati ya wachache waliochagua kufa. Alisema kwamba, sababu kubwa ya kuja ni kufa kwa ajili yetu. Alikuja kutoa uhai wake kuwa fidia ya watu wengi’ (Marko 10:45).

Yesu alisema alikufa 'kwa ajili' yetu. Neno 'kwa ajili' linamaanisha 'badala ya'. Alifanya hivyo kwa sababu alitupenda na hakutaka tulipe deni kwa ajili ya mambo yote tuliyokosa. Pale msalabani, alikua akisema, 'Nitavichukua hivyo vyote'. Alifanya kwa ajili yako, na alifanya kwa ajili yangu. Kama wewe au mimi tungekuwa ni watu pekee duniani, bado angefanya hivyo kwa ajili yetu. Mt Paul aliandika 'Mwana wa Mungu aliyenipenda hata akayatoa maisha yake kwa ajili yangu' (Wagalatia 2:20). Ni kutokana na Upendo wake kwetu ndo maana akatoa maisha yake yawe fidia.

Neno ‘fidia’ linatokea katika soko la watumwa. Mtu mwema anaweza kumnunua mtumwa na kumwacha huru—ila kwanza lazima alipe fidia. Yesu alilipa, kwa damu yake pale msalabani, alilipa fidia ili tuwekwe huru.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Why Easter?

Pasaka ina umuhimu gani? Mbona kuna shauku sana kuhusu mtu aliyezaliwa miaka 2,000 iliyopita? Mbona watu wengi wanachangamka kuhusu Yesu? Kwa nini tunamhitaji? Kwa nini alikuja? Kwa nini alikufa? Kwa nini mtu asumbuke kujua haya? Katika mpango huu wa siku tano, Nicky Gumbel anatoa majibu ya kuvutia kwa maswali hayo.

More

Tungependa kuwashukuru Alpha na Nicky Gumbel kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://alpha.org/