Kwa nini Pasaka?Mfano
Uhuru kutoka kwenye nini?
Yesu alilipa, kwa damu yake pale msalabani, fidia ili sisi tuwe huru.
Uhuru kutoka kwenye hatia
Ikiwa tunajihisi hatia au la, wote tuna hatia mbele za Mungu kwa sababu mara nyingi tumevunja sheria zake kwa mawazo, maneno au matendo yetu. Kama vile mtu akitenda kosa kuna adhabu ya kulipia, hivyo hivyo kuna adhabu ya kulipia pale tunapovunja sheria za Mungu. 'Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.' (Warumi 6:23).
Matokeo ya mambo mabaya tunayoyafanya ni kifo cha kiroho—kutengwa na Mungu milele. Wote tunapaswa kupata hiyo adhabu. Pale msalabani, Yesu alibeba adhabu kwa niaba yetu ili tupate msamaha kamili na hatia yetu kuondolewa.
Uhuru kutoka kwenye ulevi
Yesu alisema ‘ kila mtu atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.’ (Yohana 8:34). Yesu alikufa ili atuweke huru kutoka katika utumwa. Pale msalabani, nguvu ya ulevi ilivunjwa. Ingawa tunaanguka mara kwa mara, nguvu ya ulevo ilivunjwa na Yesu alipotuweka huru.
Uhuru kutoka kwenye uoga
Yesu alikuja ili 'kwa kifo chake amwangamize aliye na nguvu ya mauti--yaani Ibilisi--na kuwaacha huru wale wote ambao maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa' (Waebrania 2: 14-15). walikuwa kwenye utumwa wa hofu, ambaye ana mamlaka juu ya kifo, na hivyo awaokoe wale waliokuwa watumwa maisha yao yote kwakwa sababu ya hofu yao ya kifo’ (Waebrania 2:14-15). Hatuhitaji kuogopa mauti tena.
Kifo si mwisho kwa wale ambao Yesu aliwaweka huru. Badala yake ni njia ya kufika mbinguni, ambapo tutakuwa huru na uwepo wa dhambi. Yesu alipotuweka huru na hofu ya mauti, alituweka huru pia hofu wa mambo yote.
Kuhusu Mpango huu
Pasaka ina umuhimu gani? Mbona kuna shauku sana kuhusu mtu aliyezaliwa miaka 2,000 iliyopita? Mbona watu wengi wanachangamka kuhusu Yesu? Kwa nini tunamhitaji? Kwa nini alikuja? Kwa nini alikufa? Kwa nini mtu asumbuke kujua haya? Katika mpango huu wa siku tano, Nicky Gumbel anatoa majibu ya kuvutia kwa maswali hayo.
More