Yesu: Bendera Wetu wa UshindiMfano
Ushindi dhidi ya Hofu
Katika dunia yetu leo, ikiwa imejaa habari na kuzungukwa na taarifa mbaya zisizoisha, ni rahisi kujawa na hofu. Tunaogopa visivyojulikana, tunaogopa maumivu na hasara, tunaogopa kwa kutokuwa na kitu cha kutufanya tufanikiwe. Lakini wakati Mwokozi wetu asiye na hatia alipokufa msalabani kulipa kwa ajili ya dhambi zetu, alituonesha upendo kamili. Nguvu ya upendo ule ilishinda athari zote za dhambi na giza la ulimwenguni, ikiwamo hofu.
1 Yohana 4:18 inatuambia kwamba “ lakini pendo lililo kamili huitupa nje." Kupitia kuonesha kwake upendo pale msalabani, Yesu alipata ushindi dhidi ya hofu, na anatukaribisha kushiriki naye ushindi huo. Anataka tuishi kwa amani katika akili zetu, mioyo yetu, na roho zetu. Lakini ni juu yetu kupokea na kutembea katika nguvu ya ushindi wake. Katika Warumi 8:38, mtume Paulo alisema kwamba ameshawishika kwamba hakuna kitakachotutenganisha na upendo wa Mungu. Nasi pia tunayo nafasi kuwa imani isiyotetereka katika upendo wa Mungu kwa ajili yetu na kukaa katika amani itolewayo na upendo huo. Kama kuna wakati unatilia mashaka kiasi cha upendo wa Mungu kwako, unachotakiwa kufanya ni kuangalia msalabani.
Wakati hofu inapopiga hodi, una uchaguzi wa kufanya: hofu ikutawale, au kukumbuka tendo la ushindi na kuchagua kuamini kwamba ameshinda vita kwa amani yako. Wakati kila kitu kinaonekana kinaenda mrama katika ulimwengu wako, simama imara kwenye kweli kwamba hofu haina nguvu juu yako. Dai amani yake, na tembea kifua mbele kwamba umefunikwa na upendo wake!
Download today's image here.
Kuhusu Mpango huu
Tunapo sherehekea Pasaka, tunasherehekea ushindi mkuu katika historia. Kupitia kifo cha Yesu na kufufuka, alishinda nguvu ya dhambi na kaburi, na athari zake zote, na alichagua kushiriki ushindi huo nasi. Pasaka hii, hebu tuangalie baadhi ya ngome alizozishinda, angalia vita alivyovipiga kwa ajili yetu, na umsifu kama bendera ya ushindi wetu.
More