Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yesu: Bendera Wetu wa UshindiMfano

Jesus: Our Banner of Victory

SIKU 2 YA 7

Ushindi dhidi ya hukumu 

Moja ya malengo ya Shetani ni kutufanya sisi tuishi katika giza la hukumu ya mambo yaliyopita. Shetani anajua kwamba hata kama tunaamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, lakini bado tunabeba hukumu ya dhambi zetu, hatutaweza kupkea baraka za kweli na uhuru wa msamaha wake. Tutaishi katika kivuki cha dhambi zetu mbaya. Katika Yohana 9:5, Yesu anajitaja kama mwanga wa ulimwengu. Lakini katika Mathayo 5:14 na 16, Yesu pia anasema " Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji ukiojengwa juu ya mlima hauwezi kusitirika...vivyo hivyo, nuru yenu na iangaze kwa watu wote, wapate kuyaona matendo yenu mema na kumtukuza baba yenu wa mbinguni.” Yesu asingetegemea tuwe nuru ya utukufu wake kama asingetoa njia ya kututia katika giza la hukumu.

Zaburi 103: 10-12 inatuambia upendo wa Mungu kwetu ni mkubwa kuliko tunavyoweza kufikiria, na kwamba amezichukua dhambi mbali nasi kiasi kwamba hatuwezi kujua umbali wake. Yesu alipokufa msalabani, alichukua mzigo wa dhambi mbali na wote waaminio. Sasa tunaweza kupokea msamaha wake, kuishi bila hukumu, na kukaribishwa katika uwepo wa Mungu.

Tunapokaribia kusherehekea kufufuka kwa Yesu, hebu na tukumbuke kwamba mauti yake ilinunua siyo tuu msamaha wetu kutoka kwenye dhambi, bali pia mamlaka ya kutupa mzigo wa hukumu. Deni la dhambi yako, hata ile kubwa, limelipwa kwa damu ya Yesu. Tembea katika uhuru wake leo!

Download today's image here

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Jesus: Our Banner of Victory

Tunapo sherehekea Pasaka, tunasherehekea ushindi mkuu katika historia. Kupitia kifo cha Yesu na kufufuka, alishinda nguvu ya dhambi na kaburi, na athari zake zote, na alichagua kushiriki ushindi huo nasi. Pasaka hii, hebu tuangalie baadhi ya ngome alizozishinda, angalia vita alivyovipiga kwa ajili yetu, na umsifu kama bendera ya ushindi wetu.

More

Tungependa kushukuru Church of the Highlands kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.churchofthehighlands.com