Yesu: Bendera Wetu wa UshindiMfano
Ushindi dhidi ya aibu
Adui anapenda kuzungumza. Neno la Mungu linasema kwamba shetani huzunguka kama simba angurumae akitafuta mtu wa kummeza. Katika Ufunuo, amesemwa kama mshitaki; tunaambiwa kwamba hutushitaki mbele za Mungu usiku na mchana. Shetani ni mjanja, na anajua njia bora za kuua, kuiba na kuharibu uwezo wetu wa kimungu ni kutuwekea mzigo wa dhambi ili kutufanya siku zote tujione hatufai. Anataka tuishi katika aibu.
Unaona, hukumu ni juu ya yale tuliyofanya, lakini aibu ni kuhusu sisi ni nani. Wengi wetu tunakubali kwamba Mungu ametusamehe kwa yale tuliyotenda lakini bado tunamruhusu adui atushitaki na na kumruhusu atujaze uongo kuhusu sisi ni nani. Uongo huu unatulemaza katika kupokea na kutembea katika kusudi la Mungu katika maisha yetu. Tumeitwa kutumia karama na vipaji tulivyopewa na Mungu kuleta mabadiliko katika ulimwengu huu, lakini tusipotoka katika hukumu na kutokustahili, hatutaweza kutimiza kusudi la kuumbwa kwetu.
Yesu alipobadilisha dhambi zetu na haki yake msalabani, alitufanya wapya. Vile tulivyokuwa mwanzo hakuna tofauti na tulivyo sasa. Sisi ni watoto wa Mungu, tumesamehewa, tumefunikwa na neema, tumewezeshwa kufanya makuu kwa ajili ya utukufu wake. Sauti za aibu zinazopingana na ukweli ni uongo tuu
Juma lote hili la Pasaka, kumbuka Mungu anasema nini juu yako, mwanawe, na uchukue mateka mawazo yote ambayo hayaendani na neno lake. Yesu alikuja ili tuwe na uzima tele. Tupa mbali aibu, na tafuta utimilifu wa kusudi lako la kimungu!
Download today's image here.
Kuhusu Mpango huu
Tunapo sherehekea Pasaka, tunasherehekea ushindi mkuu katika historia. Kupitia kifo cha Yesu na kufufuka, alishinda nguvu ya dhambi na kaburi, na athari zake zote, na alichagua kushiriki ushindi huo nasi. Pasaka hii, hebu tuangalie baadhi ya ngome alizozishinda, angalia vita alivyovipiga kwa ajili yetu, na umsifu kama bendera ya ushindi wetu.
More