Injili Ulimwenguni - Sehemu 2Mfano
Yesu aponia mwana wa afia wa kifalme
Baada ya zile siku mbili, Yesu aliondoka kwenda Galilaya. (Basi Yesu mwenyewe alikuwa amesema kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.)
Alipofika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha, kwani walikuwa wameona yale aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa maana wao pia walikuwa wamehudhuria kwenye hiyo Sikukuu. Hivyo Yesu akaja tena mpaka Kana ya Galilaya, kule alikokuwa amebadili maji kuwa divai.
"Huko kulikuwako na mtu mmoja afisa wa kifalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu.
Huyo mtu aliposikia kwamba Yesu alikuwa amewasili Galilaya kutoka Uyahudi, alimwendea na kumwomba ili aje kumponya mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa.
“Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.”
“Bwana, Yule afisa wa kifalme akamwambia, "tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa.”
Yesu akamjibu, “Enenda zako, mwanao yu hai.”
Yule afisa akaamini yale maneno Yesu aliyomwambia, akaondoka akaenda zake.
"Alipokuwa bado yuko njiani, akakutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanawe yu mzima.
Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.”
Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao yu hai.” Kwa hiyo yeye, pamoja na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.
More
Tungependa kumshukuru GNPI Kenya kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/