Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2Mfano

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2

SIKU 2 YA 7

Wanafunzi wa Kwanza wa Yesu  

Siku iliyofuata, Yohana alikuwako huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili.Alipomwona Yesu akipita, akasema,

“Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!” Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, wakamfuata Yesu.Yesu akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?”

Wakamwambia,“Rabi,” (maana yake Mwalimu), “Unaishi wapi?” Yesu akawajibu,“Njoni, nanyi mtapaona!”

Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.

Andrea nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yohana aliyokuwa amesema, naye ndiye aliyemfuata Yesu.Kitu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia,“Tumemwona Masiya” (yaani Kristo).

Naye akamleta kwa Yesu.Yesu akamwangalia na kusema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa”(ambalo limetafsiriwa Petro).

Siku iliyofuata Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”

Basi Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji alikotoka Andrea na Petro. Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, 

“Tumemwona yeye ambaye Mose aliandika habari zake katika Torati na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani, Yesu wa Nazareti, mwana wa Yosefu.” Nathanaeli akauliza, 

"Je, kitu cho chote chema chaweza kutoka Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo uone.”

Yesu alipomwona Nathanaeli anakaribia, akanena habari zake akasema, 

“Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli, hana hila ndani yake.” Nathanaeli akamwuliza, 

“Umenifahamuje?” Yesu akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.” Nathanaeli akamwambia, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”

Yesu akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo.”

Ndipo akawaambia, “Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.

More

Tungependa kumshukuru GNPI Kenya kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/