Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2Mfano

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2

SIKU 5 YA 7

Mwanamke Msamaria

Mafarisayo wakasikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kubatiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana,

ingawa kwa kweli si Yesu mwenyewe aliyekuwa akibatiza, ila ni wanafunzi wake. Bwana alipojua mambo haya, aliondoka Uyahudi akarudi tena Galilaya. Wakati huo ilimlazimu apitie Samaria.

Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yosefu.

Huko ndiko kulikokuwa na kile kisima cha Yakobo. Naye Yesu alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

Mwanamke mmoja Msamaria akaja kuteka maji, Yesu akamwambia, “Naomba maji ninywe.”

(Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)

Yule mwanamke akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.

Yesu akajibu akamwambia, “Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.”

Bwana, Yule mwanamke akamjibu, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi?

Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”

Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki, ataona kiu tena.

Lakini ye yote anywaye maji nitakayompa, hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji yakibubujika uzima wa milele.”

Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuteka maji!”Yesu akamjibu, “Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa.”

Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” Yesu akamwambia, “Umesema kweli kuwa huna mume.

Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanaume unayeishi naye sasa si mume wako!”

Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii.

Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.” Yesu akamjibu,  “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”

Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. 

"Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”

Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye Masiya.” Wakati huo 

wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke.

"Lakini hakuna aliyemwuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”

Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu,

“Njoni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Masiya?”

Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu. Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau cho chote.”

Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”

Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?”

Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake.

Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ "Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa!

Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunae wafurahi pamoja.

"Hivyo kule kusema, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa.

Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”

Wasamaria wengi kutoka katika mji ule wakamwamini Yesu kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba,

“Ameniambia kila jambo nililotenda.”

"Hivyo wale Wasamaria walipomjia, wakamsihi akae kwao. Naye akakaa huko siku mbili.

Kwa sababu ya neno lake, watu wengi wakaamini. Wakamwambia yule mwanamke,"

“Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua hakika kweli ya kwamba huyu ndiye Kristo, Mwokozi wa ulimwengu.”

Andiko

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Injili Ulimwenguni - Sehemu 2

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana.

More

Tungependa kumshukuru GNPI Kenya kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org/