Kutumia muda wako kwa ajili ya MunguMfano
"Kushinda Saa"
Nimejifundisha mbinu chache kunisaidia kushinda saa. Zinaweza kuwa za manufaa kwako pia.
Nimegundua kuwa muda wangu wote ni muda wa Mungu na kuwa muda wangu wote ni wangu kwa kupewa na Yeye. Mungu ananimiliki, mimi na muda wangu. Ilhali, amenipa kiwango cha muda ambacho mimi ni msimamizi. Naweza fanya muda huo uwe muda wa kufanyia watu wengine kazi, kuwatembelea watu wengine na kadhalika, lakini ni muda ambao lazima ni uwajibikie.
Muda unaweza okolewa kwa kumakinika na kuwa na lengo. Upotezaji wa muda mkubwa hufanyika akilini mwa binadamu. Mikono yetu inaweza kuwa yenye shughuli lakini akili zetu zimezubaa. Vile vile, mikono yetu inaweza kuwa imezubaa na akili zetu zenye shughuli. Fikira zisizokuwa na maana na kujihusisha na ndoto za kijinga ni njia ambazo mawazo na fikira zinapotezwa katika muda halisi. Kulenga akili zetu kwa kazi tunayofanya—na kwa kumakinika zaidi—hufanya matumizi bora ya muda.
Akili inaweza okoa muda wa thamani uliochukuliwa na kazi za kawaida au za kiufundi. Kwa mfano, ufundi wa kuoga (mkaragazo) sio ngumu. Katika muktadha huu, akili iko huru kwa ajili ya kutatua tatizo, fikra za ubunifu, au muundo wa mandhari. Jumbe zangu nyingi na mihadhara zimetokea nikiwa bafuni nikioga. Nilipokuwa nikicheza gofu, nilipata kuwa muda niliokuwa nao kati ya shuti ulikuwa muda tosha wa kutunga jumbe akilini.
Coram deo: Kuishi mbele ya uso wa Mungu
Kuwa na ufahamu wa kule unakolenga akili yako leo. Jaribu kuokoa muda wa thamani unaotumia kwa kazi za kawaida na kazi za kiufundi kwa kufikiria mambo ya milele yenye thamani.
Hakimiliki © Huduma za Ligonier. Pata kitabu cha bure kutoka kwa R.C. Sproul Ligonier.org/freeresource.

Kuhusu Mpango huu
Ibada ya siku nne kutoka kwa R.C. Sproul, jinsi ya kutumia wakati wako kwa ajili ya Mungu. Kila Ibada inakuhimiza kuishi katika uwepo wa Mungu, chini ya mamlaka ya Mungu, kwa utukufu wa Mungu.
More
Tungepeanda kuwashukuru Ligonier Ministries kwa kutupatia mpango huu Kwa maelezo zaidi,tembelea Ligonier.ord/freeresource