Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Mipaka ina makusudi
Kukuwa na kiasi na kujidhibiti, na kuanzisha mipaka dhabiti katika maisha yetu ni baadhi ya mambo muhimu tunayoweza kufanya. Uhai ambao hauna nidhamu ni moja ambao imejazwa na kutojali.
Neno la Mungu linaweka mipaka muhimu ili kutuweka katika eneo la usalama wa Mungu. Linatuambia nini tunaweza kufanya, na kile si bora kufanya, ili kuwa salama.
Kama Wakristo tunaweza kufikiri ni aina ya kusisimua kuishi maisha ya kutojali. Tunapenda picha ya "Ndio! Ndo mimi huyo! Kuishi bila kujali! "Ni njia maarufu ya kuangalia maisha.
Lakini kwa kusema kweli, Mungu hataki tuishi kwa hali hiyo, kwa sababu ikiwa tunaishi hivyo, basi hatuna nafasi ya kujikinga na makosa.
Barabara zina mistari, moja kwa upande na moja katikati. Mstari huu hutupa nafasi kwa ajili ya usalama wetu wakati tunapoendesha gari. Ikiwa tunapita juu ya mstari upande mmoja, tutaingia shimoni. Ikiwa tunapita kwa le wa katikati, tunaweza kuuawa. Tunapenda mistari hiyo kwa sababu husaidia kutuweka salama.
Ni kama hivyo katika maisha yetu binafsi pia. Wakati tuna mipaka,na vizuizi, tunahisi vizuri zaidi na kushiriki amani ya Mungu.
La muhimu ni kwenda Neno la Mungu, ambalo ameweka mipaka yote tunayohitaji kuishi. Hebu Mungu aongoze njia yako kila siku
OMBI LA KUANZA SIKU
. Mungu, mimi ninatambua haja ya mipaka katika maisha yangu. Ninaposoma Neno lako, nionyeshe jinsi ya kutumia mipaka yako nzuri katika maisha yangu leo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili