Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Kutupa hofu nje
Nataka kuzungumza na wewe juu ya neno la herufi nne: hofu! Wengi wetu tunaweza kukumbuka wakati tulipokuwa watoto, ikiwa tulisema neno baya, mama yetu alitishia kuosha mdomo wetu kwa sabuni. Naam, kama "hofu" ni neno chafu, herufi nne, basi imani katika upendo wa Mungu ni sabuni!
Sizungumzi juu ya imani hafifu. Ninazungumzia juu ya imani yenye nguvu katika upendo wa Mungu usio na masharti, usio na ukomo, usioyumbayumba , na ulio kamilifu kwetu.
1 Yohana 4:18 inatufundisha kwamba kuelewa upendo wa Mungu kwetu kutatuokoa kutokana na hofu zetu. Sasa hii haimaanishi kwamba hatuwezi kuhisi hofu, lakini imani katika Mungu na upendo wake itatusaidia "kufanya hivyo huku tukiwa na hofu" kama tunapaswa.
Mungu anataka ujue kwamba Yeye yu pamoja nawe. Yeye atakuongoza na kukuelekeza, ili uweze kuweka ujasiri na imani yako ndani yake! Kumbuka, upendo wake ni mkamilifu, hata wakati hatuko wakamilifu. Yeye hatatupenda zaidi au kidogo kwa sababu ya makosa yetu. Je, si ni vizuri kujua kwamba Mungu anakupenda katika hali uliyo ndani?? Je! Si wazo hilo linaweza kuimarisha imani yako na kupunguza hofu yako?
Wewe na mimi tutahisi hofu mara kwa mara. Tunapofanya hivyo, tunaweza kumtazamia Mungu na kujua kwamba atatuongoza kupitia hali yoyote tunayokabiliana nao.
Ni upendo mkamilifu wa Mungu-sio ukamilifu wetu-ambao hutoa hofu kila wakati.
OMBI LA KUANZA SIKU
Mungu, upendo wako pekee undio unaweza kuondoa hofu yangu, kwa hiyo nimeweka imani yangu ndani yako. Najua kuwa uwepo wako u pamoja nami na kwamba Wewe utaniongoza kupitia hali yoyote ya kutisha inayonikabili. Ninapokea upendo wako
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili