Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Oswald Chambers: Amani - Maisha kwenye RohoMfano

Oswald Chambers: Peace - Life in the Spirit

SIKU 27 YA 30

Shetani hajawahi kuelezwa kwenye Biblia kama ana hatia kwa kutenda mambo mabaya: yeye ni kiumbe wa makosa. Wanadamu huwajibika kwa kufanya makosa, na hukosa kwa sababu ya tabia mbaya ndani yao. Maadili ya kijinga ya asili yetu inatufanya kumlaumu Shetani wakati tunajua vizuri kabisa tunatakiwa kujilaumu wenyewe; wakumlaumu ni tabia zilizopo ndani yetu.

Kuna uwezekano mkubwa Shetani anasikitika kama Roho Mtakatifu tunapoingia katika dhambi, kwa sababu yoyote. Watu wakiingia kwenye dhambi na ikamsikitisha anajua wazi kabisa kwamba watu hao watahitaji mtawala mwingine, mwokozi na mkombozi; kwa mda mrefu iwezekanavyo Shetani ataweka watu kwenye amani na umoja na maelewano mbali na Mungu, ata fanya tu (angalia Luka 11:21-22).

Maswali Ya Tafakari: Namlaumu nani kwa dhambi zangu? Shetani anapata faida gani nikiishi maisha ya maadili na usawa? Na anapoteza nini nikiharibu vibaya sana mpaka nitambue uhitaji wa amani mbali na jitihada zangu?

Nukuu kutoka saikolojia ya Kibiblia, © Discovery House Publishers
siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Oswald Chambers: Peace - Life in the Spirit

Amani: Maisha ya Roho ni hazina ya msukumo ya nukuu kutoka kwenye kazi za Oswald Chambers, mwandishi mpendwa ulimwenguni wa ibada na mwandishi wa My Utmost for His Highest. Pata mapumziko kwa Mungu na pata uelewa zaidi wa umuhimu wa amani ya Mungu kwenye maisha yako.

More

Tungependa kushukuru Huduma ya Discovery House Publishers kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.utmost.org