Zaburi 55:12-14
Zaburi 55:12-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana aliyetukana si adui; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo, ningejificha asinione. Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana. Tulipeana shauri tamu; na kutembea Nyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano.
Zaburi 55:12-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama adui yangu angenitukana, ningeweza kustahimili hayo; kama mpinzani wangu angenidharau, ningeweza kujificha mbali naye. Kumbe, lakini, ni wewe mwenzangu; ni wewe rafiki yangu na msiri wangu! Sisi tulizoea kuzungumza kirafiki; pamoja tulikwenda nyumbani kwa Mungu.
Zaburi 55:12-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana si adui aliyenitukana; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo, ningejificha asinione. Bali ni wewe, mtu mwenzangu, Rafiki yangu, niliyejuana nawe sana. Tumehusiana vizuri; na kutembea Nyumbani mwa Mungu pamoja na mkutano.
Zaburi 55:12-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia, kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu, ningejificha asinione. Kumbe ni wewe, mwenzangu, mshiriki na rafiki yangu wa karibu, ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri, tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu.