Zaburi 42:7-8
Zaburi 42:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Nimeporomoshewa mafuriko ya maji mafuriko ya maji yaja karibu nayo yaita maporomoko mapya. Mawimbi na mapigo yako yamenikumba. Mwenyezi-Mungu atanijalia fadhili zake mchana; nami nimwimbie wimbo wa sifa usiku, nimwombe Mungu anipaye uhai.
Zaburi 42:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maporomoko ya maji yako, Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu. Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami, Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.
Zaburi 42:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maboromoko ya maji yako, Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu. Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami, Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.