Zaburi 18:46-49
Zaburi 18:46-49 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu; Ndiye Mungu anipatiaye kisasi; Na kuwatiisha watu chini yangu. Huniponya na adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia, Na kuniponya na mtu wa jeuri. Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.
Zaburi 18:46-49 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu yu hai! Asifiwe mwamba wa usalama wangu; atukuzwe Mungu wa wokovu wangu. Yeye ameniwezesha kulipiza kisasi; na kuyashinda mataifa chini yangu. Ameniokoa kutoka kwa maadui zangu, akanikuza juu ya wapinzani wangu, na kunisalimisha mbali na watu wakatili. Kwa hiyo nitakutukuza kati ya mataifa, ee Mwenyezi-Mungu nitaliimbia sifa jina lako.
Zaburi 18:46-49 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA ndiye aliye hai; Na ahimidiwe mwamba wangu; Na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu; Ndiye Mungu anilipizaye kisasi; Na kuwatiisha watu chini yangu. Huniponya na adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia, Na kuniponya na mtu mjeuri. Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.
Zaburi 18:46-49 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu! Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, awatiishaye mataifa chini yangu, aniokoaye na adui zangu. Uliniinua juu ya adui zangu; uliniokoa toka kwa watu wajeuri. Kwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, Ee BWANA; nitaliimbia sifa jina lako.