Zaburi 130:1-8
Zaburi 130:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Toka upeo wa unyonge wangu, nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu. Ee Bwana, sikia sauti yangu, uitegee sikio sauti ya ombi langu. Kama, ee Mwenyezi-Mungu ungekumbuka maovu yetu nani, ee Bwana, angeweza kusalimika? Lakini kwako twapata msamaha, ili sisi tukuheshimu. Namtumainia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote; nina imani sana na neno lake. Ninamtumainia Mwenyezi-Mungu kuliko walinzi wanavyongojea pambazuko; kuliko walinzi wanavyongojea kuche asubuhi. Ee Israeli, umtumainie Mwenyezi-Mungu, maana kwake Mwenyezi-Mungu kuna fadhili, kwake kuna nguvu kubwa ya kutukomboa. Yeye atawakomboa watu wa Israeli kutoka katika maovu yao yote.
Zaburi 130:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia. Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu. BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe. Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia. Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi. Ee Israeli, umtarajie BWANA; Maana kwa BWANA kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi. Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.
Zaburi 130:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia. Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu. BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe. Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia. Nafsi yangu inamngoja Bwana, Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, Naam, walinzi waingojao asubuhi. Ee Israeli, umtarajie BWANA; Maana kwa BWANA kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi. Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.
Zaburi 130:1-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kutoka vilindini ninakulilia, Ee BWANA. Ee BWANA, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie. Kama wewe, Ee BWANA, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama? Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa. Namngojea BWANA, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu. Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi. Ee Israeli, mtumaini BWANA, maana kwa BWANA kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili. Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote.