Zaburi 105:1-3
Zaburi 105:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu, tangazeni ukuu wake; yajulisheni mataifa mambo aliyotenda! Mshangilieni, mwimbieni Mungu sifa; simulieni matendo yake ya ajabu! Jisifieni jina lake takatifu; wenye kumcha Mwenyezi-Mungu na wafurahi.
Shirikisha
Soma Zaburi 105Zaburi 105:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haleluya. Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, Wajulisheni watu matendo yake. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Yasimulieni maajabu yake yote. Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
Shirikisha
Soma Zaburi 105Zaburi 105:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haleluya. Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, Wajulisheni watu matendo yake. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi, Zitafakarini ajabu zake zote. Jisifuni kwa jina lake takatifu, Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
Shirikisha
Soma Zaburi 105