Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 105

105
Uaminifu wa Mungu kwa Israeli
1 # Isa 12:4 Haleluya.#105:1Haleluya maana yake ni, Msifuni BWANA.
Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake,
Wajulisheni watu matendo yake.
2Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini ajabu zake zote.
3Jisifuni kwa jina lake takatifu,
Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
4 # Zab 27:8 Mtakeni BWANA na nguvu zake,
Utafuteni uso wake sikuzote.
5 # Kum 8:2 Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya,
Miujiza yake na hukumu za kinywa chake.
6Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake;
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
7 # Isa 26:9 Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu;
Duniani mwote mna hukumu zake.
8 # Lk 1:72 Analikumbuka agano lake milele;
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
9 # Mwa 12:7; 17:8; 26:3 # Mwa 17:2; 22; 16; 26:3; Zab 111:5,9; Dan 9:4; Lk 1:73; Ebr 6:17 Agano alilofanya na Ibrahimu,
Na uapo wake kwa Isaka.
10 # Mwa 28:13 Alilomthibitishia Yakobo liwe amri,
Na Israeli liwe agano la milele.
11 # Mwa 15:18 Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani,
Iwe urithi wenu mliopimiwa.
12 # Mwa 34:30; Kum 7:7; Mwa 17:8; Ebr 11:9 Walipokuwa watu wawezao kuhesabiwa,
Naam, watu wachache na wageni ndani yake,
13Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa,
Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine.
14 # Mwa 12:17; 20:3-7; 35:5 Hakumwacha mtu awaonee,
Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao.
15Akisema, Msiwaguse masihi#105:15 Au, mtiwa mafuta. wangu,
Wala msiwadhuru nabii zangu.
16 # Mwa 41:53-57; 2 Fal 8:1; Law 26:26 Akaiita njaa iijilie nchi,
Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.
17 # Mwa 37:28; 45:5 Alimpeleka mtu mbele yao,
Yusufu aliuzwa utumwani.
18 # Mwa 39:20—40:15,23 Walimwumiza miguu yake kwa pingu,
Akatiwa katika minyororo ya chuma.
19Hata wakati wa kuwadia neno lake,
Ahadi ya BWANA ilimjaribu.
20 # Mwa 41:14 Mfalme alituma watu akamfungua,
Mkuu wa watu akamwachia.
21 # Mwa 41:39-41 Akamweka kuwa bwana wa nyumba yake,
Na mwenye amri juu ya mali zake zote.
22Awafunge masheki wake kama apendavyo,
Na kuwafundisha wazee wake hekima.
23 # Mwa 46:6; 47:11 Israeli naye akaingia Misri,
Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu.
24 # Kut 1:7-14; Kum 26:5; Mdo 7:17 Akawajalia watu wake wazae sana,
Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao.
25Akawageuza moyo wawachukie watu wake,
Wakawatendea hila watumishi wake.
26 # Kut 3:10—4:17; Hes 16:5 Akamtuma Musa, mtumishi wake,
Na Haruni ambaye amemchagua.
27Akaweka mambo ya ishara zake kati yao,
Na miujiza katika nchi ya Hamu.
28 # Kut 10:21-23; Zab 99:7 Alituma giza, kukafunga giza,
Wala hawakuyaasi maneno yake.
29 # Kut 7:17-21 Aliyageuza maji yao yakawa damu,
Akawafisha samaki wao.
30 # Kut 8:1-6 Nchi yao ilijaa vyura,
Vyumbani mwa wafalme wao.
31 # Kut 8:16-17,20-24 Alisema, kukaja makundi ya mainzi,
Na chawa mipakani mwao mwote.
32 # Kut 9:22-25 Badala ya mvua aliwapa mvua ya mawe,
Na moto wa miali katika nchi yao.
33Akaipiga mizabibu yao na mitini yao,
Akaivunja miti ya mipaka yao.
34 # Kut 10:12-15 Alisema, kukaja nzige,
Na tunutu wasiohesabika;
35Wakaila miche yote ya nchi yao,
Wakayala matunda ya ardhi yao.
36 # Mwa 49:3; Kut 12:29 Akawapiga wazaliwa wa kwanza katika nchi,
Malimbuko ya nguvu zao.
37 # Kut 12:33-36 Akawatoa hali wana fedha na dhahabu,
Katika kabila zao asiwepo mwenye kukwaa.
38Misri ilifurahi walipoondoka,
Maana kwa ajili yao hofu imewaangukia.
39 # Kut 13:21-22; Neh 9:12 Alitandaza wingu liwe funiko,
Na moto utoe nuru usiku.
40 # Kut 16:2-15 Walipotaka akaleta kware,
Akawashibisha chakula cha mbinguni.
41 # Kut 17:1-7; Hes 20:2-13; Neh 9:15; Isa 48:21; 1 Kor 10:4 Akaufunua mwamba, kukabubujika maji,
Yakapita pakavuni kama mto.
42Maana alilikumbuka neno lake takatifu,
Na Ibrahimu, mtumishi wake.
43Akawatoa watu wake kwa shangwe,
Na wateule wake kwa nyimbo za furaha.
44 # Kum 6:10; Yos 11:16-23; 13:7 Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu;
45 # Kum 4:1 Ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake.
Haleluya.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 105: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha