Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 105

105
Uaminifu wa Mungu kwa Israeli
1 # Isa 12:4 Haleluya.#105:1 Haleluya: maana yake ni, Msifuni BWANA.
Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake,
Wajulisheni watu matendo yake.
2Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi,
Yasimulieni maajabu yake yote.
3Jisifuni kwa jina lake takatifu,
Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
4 # Zab 27:8 Mtafuteni BWANA na nguvu zake,
Utafuteni uso wake sikuzote.
5 # Kum 8:2 Yakumbukeni matendo yake ya ajabu aliyoyafanya,
Miujiza yake na hukumu alizotoa.
6Enyi wazawa wa Abrahamu, mtumishi wake;
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
7 # Isa 26:9 Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu;
Hukumu zake ziko duniani kote.
8 # Lk 1:72 Analikumbuka agano lake milele;
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
9 # Mwa 12:7; 17:8; 26:3 Agano alilofanya na Abrahamu,
Na ahadi yake kwa Isaka.#Mwa 17:2; 22; 16; 26:3; Zab 111:5,9; Dan 9:4; Lk 1:73; Ebr 6:17
10 # Mwa 28:13 Alilomthibitishia Yakobo liwe amri,
Na Israeli liwe agano la milele.
11 # Mwa 15:18 Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani,
Kama fungu la urithi wenu.
12 # Mwa 34:30; Kum 7:7; Mwa 17:8; Ebr 11:9 Walipokuwa watu wawezao kuhesabiwa,
Naam, watu wachache na wageni katika nchi,
13Wakatangatanga toka taifa hadi taifa,
Toka ufalme mmoja hadi kwa watu wengine.
14 # Mwa 12:17; 20:3-7; 35:5 Hakumwacha mtu awaonee,
Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao.
15Akisema, Msiwaguse masihi#105:15 Au, mtiwa mafuta. wangu,
Wala msiwadhuru nabii zangu.
16 # Mwa 41:53-57; 2 Fal 8:1; Law 26:26 Akasababisha njaa katika nchi,
Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.
17 # Mwa 37:28; 45:5 Alimpeleka mtu mbele yao,
Yusufu aliuzwa utumwani.
18 # Mwa 39:20—40:15,23 Walimwumiza miguu yake kwa pingu,
Akatiwa katika minyororo ya chuma.
19Hadi wakati wa kuwadia neno lake,
Ahadi ya BWANA ilimjaribu.
20 # Mwa 41:14 Mfalme alituma watu na kumfungua,
Mkuu wa watu akamwachilia huru.
21 # Mwa 41:39-41 Akamweka kuwa mkuu wa nyumba yake,
Na mwenye mamlaka juu ya mali yake yote.
22Awaongoze maofisa wake kama apendavyo,
Na kuwafundisha wazee wake hekima.
23 # Mwa 46:6; 47:11 Israeli naye akaingia Misri,
Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu.
24 # Kut 1:7-14; Kum 26:5; Mdo 7:17 Akawajalia watu wake wazae sana,
Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao.
25Akawageuza moyo wawachukie watu wake,
Wakawatendea hila watumishi wake.
26 # Kut 3:10—4:17; Hes 16:5 Akamtuma Musa, mtumishi wake,
Na Haruni ambaye amemchagua.
27Akatenda mambo ya ishara zake kati yao,
Na miujiza katika nchi ya Hamu.
28 # Kut 10:21-23; Zab 99:7 Alituma giza, na kufanya nchi kuwa na giza,
Wakayaasi maneno yake.
29 # Kut 7:17-21 Aliyageuza maji yao yakawa damu,
Akawaua samaki wao.
30 # Kut 8:1-6 Nchi yao ilijaa vyura,
Hata nyumbani mwa wafalme wao.
31 # Kut 8:16-17,20-24 Alisema, kukaja makundi ya mainzi,
Na chawa katika nchi yao yote.
32 # Kut 9:22-25 Badala ya mvua aliwapa mvua ya mawe,
Na umeme uliomulika ghafla katika nchi yao.
33Akaipiga mizabibu yao na mitini yao,
Akaivunja miti ya nchi yao.
34 # Kut 10:12-15 Alisema, kukaja nzige,
Na tunutu wasiohesabika;
35Wakaila miche yote ya nchi yao,
Wakayala matunda ya ardhi yao.
36 # Mwa 49:3; Kut 12:29 Akawapiga wazaliwa wa kwanza katika nchi,
Malimbuko ya nguvu zao.
37 # Kut 12:33-36 Akawatoa wakiwa na fedha na dhahabu,
Katika makabila yao asiwepo mwenye kujikwaa.
38Misri ilifurahi walipoondoka,
Maana kwa ajili yao hofu imewaangukia.
39 # Kut 13:21-22; Neh 9:12 Alitandaza wingu liwe kifuniko,
Na moto ili uwaangazie usiku.
40 # Kut 16:2-15 Walimwomba naye akaleta kware,
Na kuwashibisha chakula cha mbinguni.
41 # Kut 17:1-7; Hes 20:2-13; Neh 9:15; Isa 48:21; 1 Kor 10:4 Akaufunua mwamba, kukabubujika maji,
Yakapita jangwani kama mto.
42Maana alilikumbuka neno lake takatifu,
Na Abrahamu, mtumishi wake.
43Akawatoa watu wake kwa shangwe,
Na wateule wake kwa nyimbo za furaha.
44 # Kum 6:10; Yos 11:16-23; 13:7 Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu;
45 # Kum 4:1 Ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake.
Haleluya.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 105: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha