Methali 8:1-4
Methali 8:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Sikilizeni! Hekima anaita! Busara anapaza sauti yake! Juu penye mwinuko karibu na njia, katika njia panda ndipo alipojiweka. Karibu na malango ya kuingilia mjini, mahali wanapoingia watu anaita kwa sauti: “Enyi watu wote, nawaita nyinyi! Wito wangu ni kwa ajili ya binadamu.
Methali 8:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake? Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, Penye njia panda, ndipo asimamapo. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele. Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu.
Methali 8:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Je! Hekima halii? Ufahamu hatoi sauti yake? Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia, Penye njia panda, ndipo asimamapo. Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini, Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele. Enyi watu, nawaita ninyi; Na sauti yangu ni kwa wanadamu.
Methali 8:1-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Je, hekima haitani? Je, ufahamu hapazi sauti? Juu ya miinuko karibu na njia, penye njia panda, ndipo asimamapo; kando ya malango yaelekeayo mjini, kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema: “Ni ninyi wanaume, ninaowaita; ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote.