Methali 28:1-5
Methali 28:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba. Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi; Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa Mtu mhitaji awaoneaye maskini, Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula. Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao. Watu wabaya hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao BWANA huelewa na yote.
Methali 28:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Waovu hukimbia japo hawafukuzwi na mtu, lakini waadilifu ni hodari kama simba. Taifa la fujo huzusha viongozi wengi, lakini kwa kiongozi mmoja mwenye akili na maarifa huwa na utengemano Mtu mhitaji anayewadhulumu maskini, amefanana na mvua kubwa inayoharibu mimea. Watu wanaovunja sheria huwasifu waovu, lakini wanaoishika sheria hupingana nao. Waovu hawajui maana ya haki, lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa.
Methali 28:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba. Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi; Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa Mtu mhitaji awaoneaye maskini, Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula. Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao. Watu waovu hawaelewi na haki; Bali wamtafutao BWANA huelewa na zote.
Methali 28:1-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza, bali wenye haki ni wajasiri kama simba. Wakati nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi, bali mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu. Mtu maskini amwoneaye yeye aliye maskini zaidi ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza mazao. Wale waiachao sheria huwasifu waovu, bali wale waishikao sheria huwapinga. Watu wabaya hawaelewi haki, bali wale wamtafutao BWANA wanaielewa kikamilifu.