Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 28

28
1Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu;
Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.
2Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi;
Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa
3 # Mt 18:28 Mtu mhitaji awaoneaye maskini,
Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula.
4 # 1 Fal 18:18; Mt 3:7; Efe 5:11; 1 Tim 5:20 Wao waiachao sheria huwasifu waovu;
Bali wao waishikao hushindana nao.
5 # Yn 7:17 Watu wabaya hawaelewi na hukumu;
Bali wamtafutao BWANA huelewa na yote.
6Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake,
Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri.
7Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima;
Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye.
8Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida,
Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
9 # 2 Tim 4:3; Zab 66:18; Lk 13:25-27 Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria,
Hata sala yake ni chukizo.
10 # Zab 34:9,10; Mt 6:33; Mk 10:30; Lk 18:29,30; Rum 8:32; 1 Kor 3:22,23 Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya,
Ataanguka katika rima lake mwenyewe;
Bali wakamilifu watarithi mema.
11Mtu tajiri ana hekima machoni pake mwenyewe;
Bali maskini mwenye ufahamu humchunguza sana.
12Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi;
Bali waovu waondokapo, watu hujificha.
13Afichaye dhambi zake hatafanikiwa;
Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
14Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote;
Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara.
15 # Mt 2:16 Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa;
Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini.
16Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana;
Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.
17Aliyelemewa na damu ya mtu
Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie.
18Aendaye kwa unyofu ataokolewa;
Bali mkaidi wa njia zake ataanguka mara.
19Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele;
Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.
20Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;
Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
21 # Eze 13:19 Kupendelea watu si kwema;
Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate.
22Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri;
Wala haufikiri uhitaji utakaomjilia.
23Amkemeaye mwenzake hatimaye atapata kibali;
Zaidi ya mtu ajipendekezaye kwa ulimi wake.
24Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa;
Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu.
25 # 1 Tim 6:6 Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina;
Bali amtumainiye BWANA atawandishwa.
26Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga;
Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa.
27Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu;
Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.
28Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha;
Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 28: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha