Methali 2:20-22
Methali 2:20-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa hiyo utafuata mfano wa watu wema, na kuzingatia mienendo ya waadilifu. Maana wanyofu wataipata nchi, na waaminifu watadumu ndani yake. Lakini waovu wataondolewa nchini, na wenye hila watangolewa humo.
Methali 2:20-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ili upate kwenda katika njia ya watu wema, Na kuyashika mapito ya wenye haki. Maana wanyofu watakaa katika nchi, Na wakamilifu watadumu ndani yake. Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang'olewa.
Methali 2:20-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ili upate kwenda katika njia ya watu wema, Na kuyashika mapito ya wenye haki. Maana wanyofu watakaa katika nchi, Na wakamilifu watadumu ndani yake. Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang’olewa.
Methali 2:20-22 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hivyo utatembea katika njia za watu wema na kushikamana na mapito ya wenye haki. Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi, nao wasio na lawama watabakia ndani yake. Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi, nao wasio waaminifu watangʼolewa kutoka humo.