Isaya 57:18-19
Isaya 57:18-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia. Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.
Isaya 57:18-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nimeziona njia zake, lakini nitamponya, nitamwongoza na kumrudishia upya faraja, nikiumba sifa midomoni ya waombolezaji katika Israeli. Amani, amani, kwa wale walio mbali na kwa wale walio karibu,” asema BWANA. “Nami nitawaponya.”
Isaya 57:18-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Niliiona mienendo yao, lakini nitawaponya; nitawaongoza na kuwapa faraja, nitawatuliza hao wanaoomboleza. Mimi nitawapa amani, amani kwa walio mbali na walio karibu! Mimi nitawaponya.
Isaya 57:18-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)