Kutoka 24:13-15
Kutoka 24:13-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, Mose akaondoka pamoja na Yoshua, mtumishi wake, akaenda kwenye mlima wa Mungu. Mose aliwaambia wale wazee, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Aroni na Huri wako pamoja nanyi; yeyote aliye na tatizo na awaendee wao.” Basi, Mose akaenda mlimani, na wingu likaufunika mlima.
Kutoka 24:13-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa akaondoka na Yoshua, mtumishi wake, Musa akapanda mlimani kwa Mungu. Akawaambia hao wazee, Tungojeeni hapa, mpaka tutakaporudi kwenu; na tazameni, Haruni na Huri wapo pamoja nanyi; kila mtu aliye na jambo na awaendee. Musa akapanda mlimani, lile wingu likaufunikiza mlima.
Kutoka 24:13-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Musa akaondoka na Yoshua, mtumishi wake, Musa akapanda mlimani kwa Mungu. Akawaambia hao wazee, Tungojeeni hapa, mpaka tutakaporudi kwenu; na tazameni, Haruni na Huri wapo pamoja nanyi; kila mtu aliye na neno na awaendee. Musa akapanda mlimani, lile wingu likaufunikiza mlima.
Kutoka 24:13-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Basi Mose akaondoka na Yoshua mtumishi wake, naye Mose akapanda juu kwenye mlima wa Mungu. Mose akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Aroni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na neno aweza kuwaendea wao.” Mose alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima