Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut 24

24
Damu ya Agano
1 # Kut 28:1; Law 10:1,2; Hes 11:16 Kisha BWANA akamwambia Musa, Kweeni wewe, na Haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini wa wazee wa Israeli, mkamfikilie BWANA; mkasujudie kwa mbali; 2na Musa peke yake ndiye atakayekaribia karibu na BWANA; lakini hao hawatakaribia karibu; wala hao watu hawatakwea pamoja naye. 3Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya BWANA, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena BWANA tutayatenda. 4#Kum 31:9; Mwa 28:18; 31:45Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli, 5akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia BWANA sadaka za amani za ng’ombe. 6#Ebr 9:18Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu. 7Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena BWANA tutayatenda, nasi tutatii. 8#Mt 26:28; Mk 14:24; Lk 22:20; 1 Kor 11:25; 1 Pet 1:2; Ebr 9:19-20; 10:29Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya BWANA pamoja nanyi katika maneno haya yote.
Juu ya Mlima: Utukufu wa Mungu Waonekana
9Ndipo akakwea juu, Musa, na haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini miongoni mwa wazee wa Israeli; 10#Mwa 32:30; Kut 3:6; 33:20,23; Isa 6:1,5; Yn 1:18; 1 Tim 6:16; 1 Yoh 4:12; Eze 1:26; 10:1; Ufu 4:3; Mt 17:2wakamwona Mungu wa Israeli; chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi, kama zile mbingu zenyewe kwa usafi wake. 11#Kut 19:21; Mwa 16:13; Kum 4:33; Mwa 31:54; Kut 18:12Naye hakuweka mkono wake juu ya hao wakuu wa wana wa Israeli; nao wakamwona Mungu, wakala na kunywa.
12 # Kut 32:15; Kum 5:22 BWANA akamwambia Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku; nami nitakupa mbao za mawe na ile sheria na hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe. 13#Kut 33:11Musa akaondoka na Yoshua, mtumishi wake, Musa akapanda mlimani kwa Mungu. 14Akawaambia hao wazee, Tungojeeni hapa, mpaka tutakaporudi kwenu; na tazameni, Haruni na Huri wapo pamoja nanyi; kila mtu aliye na neno na awaendee. 15#Kut 19:9; Mt 17:5Musa akapanda mlimani, lile wingu likaufunikiza mlima. 16#Kut 16:10; Hes 14:10Na huo utukufu wa BWANA ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu. 17#Ebr 12:18Na kuonekana kwake ule utukufu wa BWANA kulikuwa kama moto uteketezao, juu ya mlima machoni pa wana wa Israeli. 18#Kum 9:9Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arobaini, mchana na usiku.

Iliyochaguliwa sasa

Kut 24: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia