Kumbukumbu la Sheria 32:28-44
Kumbukumbu la Sheria 32:28-44 Biblia Habari Njema (BHN)
“Israeli ni taifa lisilo na akili, watu wake hawana busara ndani yao. Wangekuwa na hekima wangejua kwa nini walishindwa, wangeweza kuelewa mwisho wao utakuwaje. Mtu mmoja anawezaje kuwashinda watu 1,000, au watu wawili wanawezaje kuwashinda watu 10,000, isipokuwa kama Mwamba wao amewatupa, Mwenyezi-Mungu wao amewaacha? Hata adui zetu wenyewe wamekiri wazi, mwamba wao hauna nguvu kama mwamba wetu. Maana mizabibu yao ni miche ya Sodoma zimetoka katika konde za Gomora; zabibu zake ni zabibu zenye sumu, vishada vyake ni vichungu. Divai yao ni kama sumu ya nyoka, ina sumu kali ya majoka. “Je sina njia ya kuwaadhibu? Silaha zangu ninazo mkononi. Kisasi ni juu yangu, mimi nitalipiza, wakati miguu yao itakapoteleza; maana siku yao ya maafa imewadia, mwisho wao u karibu sana. Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake, na kuwahurumia watumishi wake, wakati atakapoona nguvu zao zimeishia, wala hakuna aliyebaki, mfungwa au mtu huru. Ndipo Mwenyezi-Mungu atakapowauliza watu wake, ‘Iko wapi ile miungu yenu, mwamba mlioukimbilia usalama?’ Iko wapi hiyo miungu iliyokula matoleo yenu na kunywa divai na tambiko zenu za kinywaji? Basi na iinuke, iwasaidieni; acheni hiyo iwe kinga yenu sasa! Oneni kuwa mimi ndimi Mungu na wala hakuna mwingine ila mimi. Mimi huua na kuweka hai; hujeruhi na kuponya, na hakuna awezaye kumwokoa yeyote mikononi mwangu. Nanyosha mkono wangu mbinguni, na kuapa, kwa uhai wangu wa milele, kama mkiuona upanga wangu umeremetao, na kunyosha mkono kutoa hukumu, nitawalipiza kisasi maadui zangu, nitawaadhibu wale wanaonichukia. Mishale yangu nitailevya kwa damu, upanga wangu utashiba nyama, utalowa damu ya majeruhi na mateka na adui wenye nywele ndefu. “Enyi mataifa washangilieni watu wake, maana yeye hulipiza kisasi damu ya watumishi wake, huwalipiza kisasi wapinzani wake, na kuitakasa nchi ya watu wake.” Mose alikuja mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, wakakariri maneno ya wimbo huu, ili Waisraeli wote wausikie.
Kumbukumbu la Sheria 32:28-44 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana hawa ni taifa wasio shauri, Wala fahamu hamna ndani yao. Laiti wangekuwa na akili, hata wakafahamu haya, Ili watafakari mwisho wao. Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama BWANA asingaliwatoa? Maana, Mwamba wao si kama Mwamba wetu, Hata adui zetu wenyewe ndivyo wahukumuvyo. Maana, mzabibu wao ni mzabibu wa Sodoma, Nao ni wa mashamba ya Gomora; Zabibu zao ni zabibu za uchungu, Vichala vyao ni vichungu. Mvinyo yao ni sumu ya majoka, Uchungu mkali wa nyoka. Je! Haya hayakuwekwa akiba kwangu? Na kutiwa mhuri kati ya hazina yangu? Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka. Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa, Naye atasema, Iko wapi miungu yao, Mwamba ule walioutumaini; Uliokula shahamu za sadaka zao, Na kunywa divai ya sadaka zao za kinywaji? Na waondoke na kuwasaidia ninyi; Na wawe hao himaya yenu. Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu, Maana, nainua mkono wangu mbinguni, Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele, Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, Nitawatoza kisasi adui zangu, Nitawalipa wanaonichukia. Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui. Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake; Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake, Atawatoza kisasi adui zake, Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake. Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni.
Kumbukumbu la Sheria 32:28-44 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana hawa ni taifa wasio shauri, Wala fahamu hamna ndani yao. Laiti wangekuwa na akili, hata wakafahamu haya, Ili watafakari mwisho wao. Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama BWANA asingaliwatoa? Maana, Mwamba wao si kama Mwamba wetu, Hata adui zetu wenyewe ndivyo wahukumuvyo. Maana, mzabibu wao ni mzabibu wa Sodoma, Nao ni wa mashamba ya Gomora; Zabibu zao ni zabibu za uchungu, Vichala vyao ni vichungu. Mvinyo yao ni sumu ya majoka, Uchungu mkali wa nyoka. Je! Haya hayakuwekwa akiba kwangu? Na kutiwa muhuri kati ya hazina yangu? Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka. Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa, Naye atasema, Iko wapi miungu yao, Mwamba ule walioutumaini; Uliokula shahamu za sadaka zao, Na kunywa divai ya sadaka zao za kinywaji? Na waondoke na kuwasaidia ninyi; Na wawe hao himaya yenu. Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu, Maana, nainua mkono wangu mbinguni, Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele, Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, Nitawatoza kisasi adui zangu, Nitawalipa wanaonichukia. Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui. Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake; Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake, Atawatoza kisasi adui zake, Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake. Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni.
Kumbukumbu la Sheria 32:28-44 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wao ni taifa lisilo na akili, hakuna busara ndani yao. Laiti wangekuwa na hekima wangefahamu hili, na kutambua mwisho wao utakuwa aje! Mtu mmoja angewezaje kufukuza elfu moja, au wawili kufukuza elfu kumi, kama si kwamba Mwamba wao amewauza, kama si kwamba BWANA amewaacha? Kwa kuwa mwamba wao si kama Mwamba wetu, sawasawa na vile adui zetu wanavyokiri. Mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma, na kutoka kwenye mashamba ya Gomora. Zabibu zake zimejaa sumu, na vishada vyake vimejaa uchungu. Mvinyo wao ni sumu ya nyoka, sumu yenye kufisha ya swila. “Je, hili sikuliweka akiba na kulifungia kwenye vyumba vyangu vya hazina? Ni juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza. Wakati utakapowadia, mguu wao utateleza; siku yao ya maafa ni karibu, na maangamizo yao yanawajia haraka.” BWANA atawahukumu watu wake, na kuwahurumia watumishi wake atakapoona nguvu zao zimekwisha wala hakuna yeyote aliyebaki, mtumwa au aliye huru. Atasema: “Sasa iko wapi miungu yao, mwamba walioukimbilia, miungu wale waliokula mafuta ya dhabihu zao na kunywa mvinyo wa sadaka zao za vinywaji? Wainuke basi, wawasaidie! Wawapeni basi ulinzi! “Tazama basi, Mimi mwenyewe, Mimi Ndiye! Hakuna mungu mwingine ila Mimi. Mimi ninaua na Mimi ninafufua, Mimi nimejeruhi na Mimi nitaponya, wala hakuna awezaye kuokoa kutoka mkononi mwangu. Ninainua mkono wangu kuelekea mbinguni na kusema: Hakika kama niishivyo milele, wakati ninapounoa upanga wangu unaometameta na mkono wangu unapoushika ili kutoa hukumu, nitalipiza kisasi juu ya adui zangu na kuwalipiza wale wanaonichukia. Nitailevya mishale yangu kwa damu, wakati upanga wangu ukitafuna nyama: damu ya waliochinjwa pamoja na mateka, vichwa vya viongozi wa adui.” Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake, kwa kuwa atailipiza damu ya watumishi wake, atalipiza kisasi juu ya adui zake na kufanya upatanisho kwa ajili ya nchi na watu wake. Mose na Yoshua mwana wa Nuni wakaja, wakanena maneno yote ya wimbo watu wakiwa wanasikia.