Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu la Torati 32

32
1 # Zab 50:4; Isa 1:2; Yer 2:12; 6:19 Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena;
Na nchi isikie maneno ya kinywa changu.
2 # 2 Sam 23:4; Ayu 29:22,23; Isa 55:10; Hos 6:4; 14:5; 1 Kor 3:6,8; Ebr 6:7; Zab 72:6 Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua,
Maneno yangu yatatona-tona kama umande;
Kama manyunyu juu ya majani mabichi;
Kama matone ya mvua juu ya mimea.
3Maana nitalitangaza Jina la BWANA;
Mpeni ukuu Mungu wetu.
4 # 2 Sam 22:31; Dan 4:37; Yer 10:10; Ayu 34:10 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu;
Maana, njia zake zote ni haki.
Mungu wa uaminifu, asiye na uovu,
Yeye ndiye mwenye haki na adili.
5Wametenda mambo ya uharibifu,
Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao;
Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka.
6 # Zab 116:12; Isa 63:16; 2 Sam 7:23; Zab 74:2 Je! Mnamlipa BWANA hivi,
Enyi watu wapumbavu na ujinga?
Je! Yeye siye baba yako aliyekununua?
Amekufanya, na kukuweka imara.
7Kumbuka siku za kale,
Tafakari miaka ya vizazi vingi;
Mwulize baba yako, naye atakuonesha;
Wazee wako, nao watakuambia.
8 # Mdo 17:26; Zek 9:2; Mwa 11:8 Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao,
Alipowabagua wanadamu,
Aliweka mipaka ya watu
Kwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.
9 # 1 Sam 10:1 Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake,
Yakobo ni kura ya urithi wake.
10 # Kum 4:36; Neh 9:20; Zab 32:7,10; 147:19,20; Rum 2:18; 3:2; Zab 17:8; Mit 7:2 Alimkuta katika nchi ya ukame,
Na katika jangwa tupu litishalo;
Alimzunguka, akamtunza;
Akamhifadhi kama mboni ya jicho;
11Mfano wa tai ataharikishaye kioto chake;
Na kupapatika juu ya makinda yake,
Alikunjua mbawa zake, akawatwaa,
Akawachukua juu ya mbawa zake;
12BWANA peke yake alimwongoza,
Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye.
13 # Isa 58:14; Ayu 29:6 Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka,
Naye akala mazao ya mashamba;
Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini,
Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;
14 # Zab 147:14; Mwa 49:11; Mt 26:28,29; Yn 6:55,56 Siagi ya ng'ombe, na maziwa ya kondoo,
Pamoja na mafuta ya wana-kondoo,
Kondoo dume wa Kibashani, na mbuzi,
Na unono wa ngano iliyo nzuri;
Ukanywa divai, damu ya mizabibu.
15 # Isa 1:4; Zab 89:26 Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke;
Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda;
Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya,
Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
16Wakamtia wivu kwa miungu migeni,
Wakamkasirisha kwa machukizo.
17 # 1 Kor 10:20 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu,
Kwa miungu wasiyoijua,
Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu,
Ambayo baba zenu hawakuiogopa.
18Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa,
Mungu aliyekuzaa umemsahau.
19BWANA akaona, akawachukia,
Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake.
20 # Mt 17:17 Akasema, Nitawaficha uso wangu,
Nitaona mwisho wao utakuwaje;
Maana, ni kizazi cha ukaidi mwingi,
Watoto wasio imani ndani yao.
21 # 1 Kor 10:22; Rum 10:19; 1 Sam 12:21 Wamenitia wivu kwa kisicho Mungu;
Wamenikasirisha kwa ubatili wao;
Nami nitawatia wivu kwa wasio watu,
Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo.
22 # Omb 4:11 Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu,
Unateketea hata chini ya kuzimu,
Unakula dunia pamoja na mazao yake,
Unaunguza misingi ya milima.
23Nitaweka madhara juu yao chungu chungu;
Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe;
24Watakonda kwa njaa, wataliwa na makaa ya moto,
Na uharibifu mkali;
Nitawapelekea meno ya wanyama wakali,
Pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini.
25 # Omb 1:20 Nje upanga utawafifiliza
Na ndani ya vyumba, utisho;
Utaangamiza mvulana na msichana,
Anyonyaye pamoja na mwenye mvi,
26Nilisema, Ningewatawanyia mbali,
Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu;
27 # Zab 140:8 Isipokuwa niliogopa makamio ya adui,
Adui zao wasije wakafikiri uongo,
Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka,
Wala BWANA hakuyafanya haya yote.
28Maana hawa ni taifa wasio shauri,
Wala fahamu hamna ndani yao.
29 # Zab 81:13 Laiti wangekuwa na akili, hata wakafahamu haya,
Ili watafakari mwisho wao.
30 # Yos 23:10; Zab 44:12 Mmoja angefukuzaje watu elfu,
Wawili wangekimbizaje elfu kumi,
Kama Mwamba wao asingaliwauza,
Kama BWANA asingaliwatoa?
31 # 1 Sam 4:8; Yer 40:3 Maana, Mwamba wao si kama Mwamba wetu,
Hata adui zetu wenyewe ndivyo wahukumuvyo.
32Maana, mzabibu wao ni mzabibu wa Sodoma,
Nao ni wa mashamba ya Gomora;
Zabibu zao ni zabibu za uchungu,
Vichala vyao ni vichungu.
33Mvinyo yao ni sumu ya majoka,
Uchungu mkali wa nyoka.
34 # Ayu 14:17 Je! Haya hayakuwekwa akiba kwangu?
Na kutiwa mhuri kati ya hazina yangu?
35 # Rum 12:19; 13:4; Ebr 10:30; Zab 94:1 Kisasi ni changu mimi, na kulipa,
Wakati itakapoteleza miguu yao;
Maana siku ya msiba wao imekaribia,
Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.
36 # Zab 135:14; Amu 2:18; Zab 90:13; 105:45; Yer 31:20; Yoe 2:14 Kwa kuwa BWANA atawaamua watu wake,
Atawahurumia watumwa wake,
Aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka,
Na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa,
37 # Amu 10:14; 2 Fal 3:13; Yer 2:28 Naye atasema, Iko wapi miungu yao,
Mwamba ule walioutumaini;
38Uliokula shahamu za sadaka zao,
Na kunywa divai ya sadaka zao za kinywaji?
Na waondoke na kuwasaidia ninyi;
Na wawe hao himaya yenu.
39 # Isa 41:4; 45:5; 46:4; 1 Sam 2:6; 2 Fal 5:7; Ayu 5:18; Zab 68:20; Isa 43:13; Hos 6:1 Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye,
Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi;
Naua Mimi, nahuisha Mimi,
Nimejeruhi, tena naponya;
Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,
40 # Kut 6:8 Maana, nainua mkono wangu mbinguni,
Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele,
41Nikiunoa upanga wangu wa umeme,
Mkono wangu ukishika hukumu,
Nitawatoza kisasi adui zangu,
Nitawalipa wanaonichukia.
42 # Ayu 13:24 Nitailevya mishale yangu kwa damu,
Na upanga wangu utakula nyama;
Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara,
Katika vichwa vya wakuu wa adui.
43 # Rum 15:10; Ufu 19:2; 6:10; Zab 85:1 Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake;
Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake,
Atawatoza kisasi adui zake,
Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake.
44Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni. 45Musa akamaliza kuwaambia Israeli wote maneno haya yote; 46akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii. 47#Mit 3:2; Rum 10:5 Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.
Utabiri wa kifo cha Musa
48 # Hes 27:12-14; Kum 3:23-27 BWANA akasema na Musa siku iyo hiyo, akamwambia, 49Kwea katika mlima huu wa Abarimu, mpaka kilima cha Nebo, kilicho katika nchi ya Moabu, kuelekea Yeriko; ukaangalie nchi ya Kanaani niwapayo wana wa Israeli kuimiliki; 50ukafe katika kilima, huko ukweako, ukusanywe uwe pamoja na jamaa zako; kama alivyokufa nduguyo Haruni katika mlima wa Hori, akakusanywa awe pamoja na watu wake; 51#Hes 20:11 kwa sababu mlinikosa ninyi juu yangu katikati ya wana wa Israeli katika maji ya Meriba huko Kadeshi, katika bara ya Sini; kwa kuwa hamkunitakasa katikati ya wana wa Israeli. 52Kwani utaiona hiyo nchi mbele yako, lakini hutakwenda huko kuingia hiyo nchi niwapayo wana wa Israeli.

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha