Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu la Sheria 32:28-44

Kumbukumbu la Sheria 32:28-44 BHN

“Israeli ni taifa lisilo na akili, watu wake hawana busara ndani yao. Wangekuwa na hekima wangejua kwa nini walishindwa, wangeweza kuelewa mwisho wao utakuwaje. Mtu mmoja anawezaje kuwashinda watu 1,000, au watu wawili wanawezaje kuwashinda watu 10,000, isipokuwa kama Mwamba wao amewatupa, Mwenyezi-Mungu wao amewaacha? Hata adui zetu wenyewe wamekiri wazi, mwamba wao hauna nguvu kama mwamba wetu. Maana mizabibu yao ni miche ya Sodoma zimetoka katika konde za Gomora; zabibu zake ni zabibu zenye sumu, vishada vyake ni vichungu. Divai yao ni kama sumu ya nyoka, ina sumu kali ya majoka. “Je sina njia ya kuwaadhibu? Silaha zangu ninazo mkononi. Kisasi ni juu yangu, mimi nitalipiza, wakati miguu yao itakapoteleza; maana siku yao ya maafa imewadia, mwisho wao u karibu sana. Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake, na kuwahurumia watumishi wake, wakati atakapoona nguvu zao zimeishia, wala hakuna aliyebaki, mfungwa au mtu huru. Ndipo Mwenyezi-Mungu atakapowauliza watu wake, ‘Iko wapi ile miungu yenu, mwamba mlioukimbilia usalama?’ Iko wapi hiyo miungu iliyokula matoleo yenu na kunywa divai na tambiko zenu za kinywaji? Basi na iinuke, iwasaidieni; acheni hiyo iwe kinga yenu sasa! Oneni kuwa mimi ndimi Mungu na wala hakuna mwingine ila mimi. Mimi huua na kuweka hai; hujeruhi na kuponya, na hakuna awezaye kumwokoa yeyote mikononi mwangu. Nanyosha mkono wangu mbinguni, na kuapa, kwa uhai wangu wa milele, kama mkiuona upanga wangu umeremetao, na kunyosha mkono kutoa hukumu, nitawalipiza kisasi maadui zangu, nitawaadhibu wale wanaonichukia. Mishale yangu nitailevya kwa damu, upanga wangu utashiba nyama, utalowa damu ya majeruhi na mateka na adui wenye nywele ndefu. “Enyi mataifa washangilieni watu wake, maana yeye hulipiza kisasi damu ya watumishi wake, huwalipiza kisasi wapinzani wake, na kuitakasa nchi ya watu wake.” Mose alikuja mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, wakakariri maneno ya wimbo huu, ili Waisraeli wote wausikie.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kumbukumbu la Sheria 32:28-44