Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 1:35-54

1 Mambo ya Nyakati 1:35-54 Biblia Habari Njema (BHN)

Wana wa Esau walikuwa Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora. Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna na Amaleki. Wana wa Reueli walikuwa Nahathi, Zera, Shama na Miza. Wana wa Seiri walikuwa Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani. Wana wa Lotani walikuwa wawili: Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna. Wana wa Shobali walikuwa Alvani, Manahathi, Ebali, Shefi na Onamu. Wana wa Sibeoni walikuwa Aya na Ana. Mwana wa Ana alikuwa Dishoni; na wana wa Dishoni walikuwa Hamrani, Eshbani, Ithrani na Kerani. Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani na Akani; na wana wa Dishoni walikuwa Usi na Arani. Wafuatao ndio wafalme waliotawala nchi ya Edomu kabla mfalme yeyote hajatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu, akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba. Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra alitawala badala yake. Yobabu alipofariki, Hushamu wa nchi ya Watemi alitawala badala yake. Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi alitawala badala yake, makao yake makuu yakiwa katika mji wa Avithi. Huyu ndiye aliyewapiga na kuwashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu. Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka alitawala badala yake. Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ulio karibu na mto Eufrate, alitawala badala yake. Shauli alipofariki, Baal-hanani mwana wa Akbori alitawala badala yake. Baal-hanani alipofariki, Hadadi kutoka Pai alitawala badala yake na jina la mkewe Akbori lilikuwa Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. Naye Hadadi akafariki. Wakuu wa makabila ya Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi, Oholibama, Ela, Pinoni, Kenazi, Temani, Mibsari, Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.

1 Mambo ya Nyakati 1:35-54 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora. Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki. Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza. Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni dada yake Lotani. Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana. Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani. Basi hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu, kabla hajatawala mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akatawala badala yake. Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akatawala badala yake. Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akatawala badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akatawala badala yake. Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akatawala badala yake. Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akatawala badala yake. Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akatawala badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi; na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni; na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari; na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.

1 Mambo ya Nyakati 1:35-54 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora. Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki. Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza. Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni umbu lake Lotani. Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana. Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani. Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akamiliki badala yake. Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akamiliki badala yake. Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akamiliki badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akamiliki badala yake. Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akamiliki badala yake. Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akamiliki badala yake. Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akamiliki badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi; na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni; na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari; na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.

1 Mambo ya Nyakati 1:35-54 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Wana wa Esau walikuwa: Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora. Wana wa Elifazi walikuwa: Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi; Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki. Wana wa Reueli walikuwa: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Wana wa Seiri walikuwa: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani. Wana wa Lotani walikuwa wawili: Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna. Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu. Wana wa Sibeoni walikuwa: Aiya na Ana. Mwana wa Ana alikuwa: Dishoni. Nao wana wa Dishoni walikuwa: Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani. Wana wa Eseri walikuwa: Bilhani, Zaavani na Akani. Wana wa Dishani walikuwa: Usi na Arani. Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli: Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba. Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake. Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake. Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi. Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake. Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake. Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake. Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. Naye Hadadi pia akafa. Wakuu wa Edomu walikuwa: Timna, Alva, Yethethi, Oholibama, Ela, Pinoni, Kenazi, Temani, Mibsari, Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.