1 Mambo ya Nyakati 1:35-54
1 Mambo ya Nyakati 1:35-54 SRUV
Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora. Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki. Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza. Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni dada yake Lotani. Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana. Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani. Basi hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu, kabla hajatawala mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akatawala badala yake. Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akatawala badala yake. Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akatawala badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akatawala badala yake. Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akatawala badala yake. Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akatawala badala yake. Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akatawala badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi; na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni; na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari; na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.