Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 1

1
Toka Adamu hadi Abrahamu
1 # Mwa 4:25; 5:3,9 Adamu, na Sethi, na Enoshi; 2na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi; 3#Yud 1:14 na Henoko, na Methusela, na Lameki; 4na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi.
5 # Mwa 10:2 Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. 6Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. 7Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani.
8 # Mwa 16:0 Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. 9Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani. 10#Mwa 10:8,13 Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. 11Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, 12#Mwa 10:14; Kum 2:23; Yer 47:4; Amo 9:7 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. 13Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; 14na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; 15na Mhivi, na Mwarki, na Msini; 16na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi.
17 # Mwa 9:23,26; 10:22; 11:10 Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. 18Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. 19Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. 20Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; 21na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; 22na Obali, na Abimaeli, na Sheba; 23na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
24 # Mwa 11:10; Lk 3:36 Shemu, na Arfaksadi, na Sala; 25#Mwa 11:15; Hes 24:24; Lk 3:35 na Eberi, na Pelegi, na Reu; 26na Serugi, na Nahori, na Tera; 27#Mwa 17:5; 2 Nya 20:7; Neh 9:7; Isa 41:8; 51:2; Rum 4:16; Yak 2:23 na Abramu, naye ndiye Abrahamu.
Toka Abrahamu hadi Yakobo
28 # Mwa 21:2,3; 16:11,15 Wana wa Abrahamu; Isaka, na Ishmaeli.
29 # Mwa 25:13-16 Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu; 30#Mwa 25:15 na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema; 31na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32 # Mwa 25:1,2 Na wana wa Ketura, suria yake Abrahamu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani. 33Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura.
34 # Mwa 21:2,3; 25:25 Na Abrahamu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.
35 # Mwa 36:9,10; Kum 2:22; Mal 1:2,3; Rum 9:13; Ebr 12:16 Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora. 36#Mwa 36:11 Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki. 37Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza. 38#Mwa 36:20 Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani. 39#Mwa 36:22 Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni dada yake Lotani. 40#Mwa 36:23 Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana. 41#Mwa 36:25,26 Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. 42#Mwa 36:27 Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani.
43 # Mwa 36:31; 49:10 Basi hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu, kabla hajatawala mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. 44Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akatawala badala yake. 45Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akatawala badala yake. 46#1 Fal 11:14 Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akatawala badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. 47Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akatawala badala yake. 48#Mwa 36:37 Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akatawala badala yake. 49Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akatawala badala yake. 50#Mwa 36:39 Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akatawala badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. 51#Mwa 36:40; Kut 15:15 Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi; 52na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni; 53na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari; 54na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mambo ya Nyakati 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia