1 Nyakati 1:35-54
1 Nyakati 1:35-54 NEN
Wana wa Esau walikuwa: Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora. Wana wa Elifazi walikuwa: Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi; Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki. Wana wa Reueli walikuwa: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Wana wa Seiri walikuwa: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani. Wana wa Lotani walikuwa wawili: Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna. Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu. Wana wa Sibeoni walikuwa: Aiya na Ana. Mwana wa Ana alikuwa: Dishoni. Nao wana wa Dishoni walikuwa: Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani. Wana wa Eseri walikuwa: Bilhani, Zaavani na Akani. Wana wa Dishani walikuwa: Usi na Arani. Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli: Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba. Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake. Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake. Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi. Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake. Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake. Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake. Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. Naye Hadadi pia akafa. Wakuu wa Edomu walikuwa: Timna, Alva, Yethethi, Oholibama, Ela, Pinoni, Kenazi, Temani, Mibsari, Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.