Wimbo Ulio Bora 7:10-12
Wimbo Ulio Bora 7:10-12 BHN
Mimi ni wake mpenzi wangu, naye anionea sana shauku. Njoo ewe mpenzi wangu, twende mashambani, twende zetu tukalale huko vijijini. Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu, tukaone kama imeanza kuchipua, na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua, pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua. Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.