Wimbo Ulio Bora 7:10-12
Wimbo Ulio Bora 7:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi ni wake mpenzi wangu, naye anionea sana shauku. Njoo ewe mpenzi wangu, twende mashambani, twende zetu tukalale huko vijijini. Tutaamka mapema, twende kwenye mashamba ya mizabibu, tukaone kama imeanza kuchipua, na kama maua ya zabibu yamekwisha kuchanua, pia kama mikomamanga imeanza kutoa maua. Huko ndiko nitakapokupatia pendo langu.
Wimbo Ulio Bora 7:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu. Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji. Twende mapema hadi mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabibu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa upendo wangu.
Wimbo Ulio Bora 7:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu. Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji. Twende mapema hata mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabihu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa pambaja zangu.
Wimbo Ulio Bora 7:10-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mimi ni mali ya mpenzi wangu, nayo shauku yake ni juu yangu. Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani, twende tukalale huko vijijini. Hebu na twende mapema katika mashamba ya mizabibu tuone kama mizabibu imechipua, kama maua yake yamefunguka, na kama mikomamanga imetoa maua: huko nitakupa penzi langu.