Wim 7:10-12
Wim 7:10-12 SUV
Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu. Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji. Twende mapema hata mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabihu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa pambaja zangu.