Zaburi 9:1-4
Zaburi 9:1-4 BHN
Nitakushukuru Mungu kwa moyo wangu wote; nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. Nitafurahi na kushangilia kwa sababu yako; nitaliimbia sifa jina lako, ewe Mungu Mkuu. Wakati ulipotokea, maadui zangu walirudi nyuma, walijikwaa na kuangamia. Umenitetea kuhusu kisa changu cha haki; umeketi katika kiti chako cha enzi, ukatoa hukumu iliyo sawa.