Zaburi 9:1-4
Zaburi 9:1-4 NEN
Ee BWANA, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. Nitafurahi na kushangilia ndani yako. Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana. Adui zangu wamerudi nyuma, wamejikwaa na kuangamia mbele zako. Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu; umeketi kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki.