Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 72:12-19

Zaburi 72:12-19 BHN

Anamkomboa fukara anayemwomba, na maskini asiye na wa kumsaidia. Anawahurumia watu dhaifu na fukara, anayaokoa maisha yao wenye shida. Anawatoa katika udhalimu na ukatili, maana maisha yao ni ya thamani kubwa kwake. Mfalme na aishi maisha marefu; apokee zawadi ya dhahabu kutoka Sheba; watu wamwombee kwa Mungu daima, na kumtakia baraka mchana kutwa. Nchi na izae nafaka kwa wingi, vilima vijae mavuno kama ya Lebanoni, na watu mijini wastawi kama nyasi. Jina la mfalme litukuke daima; fahari yake idumu pindi liangazapo jua. Kwake mataifa yote yabarikiwe; watu wote wamwite mbarikiwa! Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye peke yake hufanya miujiza. Jina lake tukufu na litukuzwe milele; utukufu wake ujae ulimwenguni kote! Amina, Amina!

Soma Zaburi 72