Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 72:12-19

Zaburi 72:12-19 SRUV

Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi. Atawahurumia wanyonge na maskini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa. Atawakomboa kutoka kwa maonevu na udhalimu, Maana damu yao ina thamani machoni pake. Na aishi maisha marefu! Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa. Na uwepo wingi wa nafaka Katika ardhi juu ya milima; Matunda yake na yawayewaye kama ilivyo katika milima ya Lebanoni, Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi. Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua, umaarufu wake uwepo; Mataifa yote na wabarikiwe katika yeye, Na kumwita heri. Na ahimidiwe BWANA, Mungu, Mungu wa Israeli, Atendaye miujiza Yeye peke yake; Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.

Soma Zaburi 72